Upara (Swahili language)
UPARA
ni hali ya mtu kutokuwa na nywele au ukosefu wa nywele mahali ambapo mtu huyo aliwahi kuwa na nywele na mara nyingi hasa kichwani ,
pia upara kawaida zaidi ni upungufu wa nywele unatakaokuwa unawatokea hatua kwa hatua binadamu ambao Ni wanaume ,wanawake pamoja na viumbe hai.
SABABU 3 ZA UPARA
(1)Kuharibika / kuathiriwa kwa seli za mwilini , ambazo ni white blood cell zitakapokuwa zimeathiriwa au zimevamiwa ambazo zipo kwajili ya kupigana na magonjwa na matokeo yake tutaoneshwa kwa kukosekana kwa nywele yako.
(2)HOMONI YA DHT
Mabadiliko ya homoni yatakayoweza kusababishwa na Ujauzito,
Kujifungua,
Komahedhi,
Magonjwa ya tezi ya thyroid,
Kwani hizi ni homoni zitakazokuwa na msukumo wa nguvu za ngono ,
Ukuaji wa nywele za mwilini na usoni ,
ambazo zitaweza kuathiri vibaya tezi ,
kibofu,
Pamoja na nywele za kichwani.
Namna gani ambavo homoni DHT itakavyofanya ni kwamba homoni DHT itasababisha mchakato wa ukondaji wa nywele na
Kupitia mchakato huo wa ukondaji wa nywele, upana wa mzizi wa nywele huendelea kupungua kitaratibu hadi nywele kwenye ngozi ya kichwa kufanana na manyoya hafifu au hata kutoweka kabisa.
Ila pia upara husababishwa kuzidi kwa hormone ya testosterone, ndio maana kipara mara nyingi , Ila pia
Tafiti zinaonyesha, kuota upara huambatana na kiwango kikubwa cha homoni ya 'testosterone' kwenye shina linalozalisha nywele lakini hata hivyo kiwango kiwango kilicho kwenye damu huwa cha kawaida
KURITHI
Upara wa wanaume hurithiwa kwenye jeni zinazotoka kwa mama na baba,
mara nyingi upara huu hutokea jinsi umri unavyoongezeka kwa mwanaume au mwanamke.
lliaminika awali kuwa upara ulirithiwa kutoka kwa babu wa ukoo wa mama.
Ingawa pana misingi ya imani hii, wazazi wote huchangia uwezekano wa vizalia wao kupoteza nywele.
Zifutazo ni sababu nyinginezo kwa nini nywele zako zitanyonyoka(UPARA)
1. Stress
Kila aina ya maumivu yatakayoneka mwilini au kihisia zaidi itaweza kusababisha kunyonyoka kwa nywele.
Mfano ,wa ajali ya gari au kufanyiwa upasuaji vinaweza kukusababishia stress ambayo itakuletea kunyonyoka kwa nywele zako.
Hisia za stress hazisababishi kunyonyoka kwa nywele lakini inaweza kutokea pale unapokuwa katika wakati mgumu kisaikolojia kama vile kumpoteza mtu wako wa karibu kutokana na kifo au utakapoachwa kimapenzi.
Hata hivyo,Baada ya wakati huo mgumu, nywele zako zitaanza kuota tena baada ya miezi sita endapo utaamua kupunguza kuwa na stress.
2. Homoni,
Kunyonyoka kwa nywele kutaweza kuwatokea wanawake walio katika menopause kutokana na kubadilika kwa viwango vya homoni.
Itaweza kutokea pia kwa wanawake wanaotumia vidonge vya uzazi wa mpango hususani watakapokuwa wana ashirisha mara kwa mara zoezi la kutumia vidonge hivyo.
Utashauriwa kama utatumia vidonge vya uzazi wa mpango, basi hakikisha utatakiwa kuzingatia ratiba na usiahirishe hata mara moja.
3. Ukosefu wa Protini au Hamirojo,
Ukosefu wa protini utaweza kudhoofisha ukuaji wa nywele au kusababisha kunyonyoka kwa nywele kabisa na hatimaye kuwa na kipara kabisa.
4. Ujauzito
Ujauzito ni miongoni mwa mambo yatakayo leta physical stresses na pia huleta mabadiliko ya homoni.
Kunyonyoka kwa nywele hutokea baada ya zoezi la kujifungua.
5. Kurithi
Kama mmoja kati ya wazazi wako au babu zako wa upande wa baba au mama aliwahi kuwa na tatizo la kunyonyoka nywele au kuwa na kipara kabisa, basi kutakuwa uwezekano mkubwa sana kwa jambo hilo kutokea kwako pia kwa sababu za urithi.
Hakuna maelezo yoyote ya kitabu kuhusu jinsi ya kukinga suala hili , hata hivyo utaweza kujaribu kutumia vyakula na dawa mbalimbali bila kujali sababu iliyo fanya unyonyoke nywele au kuwa na kipara,na hapa itamanisha kitaalamu mtua atatakiwa awe amezaliwa bila nywele.
6. Vinasaba vya kiume
Tafiti mbalimbali za kisayansi zinaonyesha kuwa, wanaume wengi wana anza kuonyesha dalili za kunyonyoka mwele wakiwa na umri wa kuanzia miaka sitini ( 60) na kuendelea.
kama wewe ni mwanaume mwenye umri wa kuanzia miaka 60 na kuendelea na nywele zako zimeanza kuonyesha dalili za kunyonyoka, huna haja ya kupanic wala kutafuta tiba, kwani suala hilo ni la kawaida kabisa kwa wanaume wenye umri wako.
7. Anemia
Anemia husababishwa na ukosefu wa madini ya chuma katika damu.
Watu wengi watakaosumbuliwa na tatizo hili (anemia ) watakuwa na uwezekano wa kunyonyoka kwa nywele.
Hata hivyo, ili kupambana na tatizo hili utakachotakiwa kufanya ni kuzingatia matumizi ya vyakula vyenye madini ya chuma katika mlo wako.
8. Matumizi ya vitamin A kupita kiasi.
Malimbikizo ya vitamin A mwilini husababisha kunyonyoka kwa nywele.
Hata hivyo kunyonyoka kwa nywele kutako sababishwa na malimbikizo ya vitamin A mwilini huwa ni kwa muda tu.
Nywele zako zitarejea katika hali yake ya kawaida utakapo punguza matumizi ya vyakula vyenye vitamin A kwa wingi kupita kiasi kwa sababu mwili wako utaweza kubalance vitamin zote mwilini.
9. Kupunguza uzito kwa haraka.
Kupungua uzito kwa haraka kutaweza kukufurahisha.
Lakini hata hivyo, hii itaweza kukusababishia kunyonyoka kwa nywele kutokana na stress zitakazokuwa zimesababishwa katika mwili wako.
10. Matatizo kwenye tezi aina ya thyroid ( Thyroid Gland )
Thyroid gland itahusika na michakato mbalimbali katika mwili wa mwanadamu ikiwemo ukuaji wa nywele.
Kama tezi hii haizalishi homoni za kutosha, itaweza kusababisha kunyonyoka kwa nywele. Ukiwa katika situation hii, unashauriwa kumuona daktari kwa ushauri zaidi.
Kuna sababu nyingi zitakazoweza kupelekea kupotea kwa nywele(UPARA) kama vile ,
a)Sababu za kimazingira,
b)Kuzeeka,
c)Msongo wa mawazo (stress),
d)Kuvuta sigara kupita kiasi,
e)Lishe duni,
f)Homoni kutokuwa sawa,
g) Kurithi
h) Maambukizi kwenye ngozi ya kichwa
i)Matumizi yasiyo sahihi ya vipodozi vya nywele
j)Baadhi ya dawa za hospitali
k)Matatizo katika kinga ya mwili
l)Upungufu wa madini chuma
m)Na magonjwa mengine sugu
Thanks🤓🤓
ReplyDelete